Thursday, April 21, 2011

Migomo vyuo vikuu hadi lini

By Martha Mboma
Migomo  ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini imezidi kuongezeka kadri ya siku zinavyoenda na migomo hiyo inayotoke katika vyuo hivi vikuu nchini inatokana na sababu mbalimbali mpaka wanafunzi hao kugoma ivo serikali iangalie tatizo hili vizuri ili kuweza kupatia suluhu.
Katika migomo hii ya wanafunzi wa vyuo vikuu imekuwa ikitokana na sababu mbalimbali katika mgomo wa wanafunzi wa UDOM huu ulianzishwa na wanafunzi wa Kitivo cha sayansi na jamii ambapo walikuwa wakidai kuwa wkutoruhusiwa kufanya mazoezi kwa vitendo kuwa na miundo mbinu mibovu vyakula vibovu na  uhaba wa maji katika chuo chao ndiko kulipelekea wanafunzi hao kugoma katia chuo hicho licha ya kwamba wanafunzi hao wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali ya kutokuwa na wahadhiri wakutosha na wanafunzi kutopata mikopo yao katika muda muafaka na hivyo kusababisha wao kugoma na kupoteza mda mwingi wa masomo yao  na baadhi ya wanafunzi wenzao kuwekwa ndani baada ya mgomo huu.
Baada ya waziri Mizengo Kayanza Peter Pinda kuongea na na wahadhiri  na wanafunz wa chuo kikuu cha UDOM na kuweza kusawazisha mambo wanafunzi hao walisitisha mgomo na kuhaidiwa watatekelezewa madai yao na wahadhiri kuendelea kufundishi uku katika chuo kikuu Makumira kilichopo jijini Arusha mambo yalkuwa mabaya baada ya wanafunzi hao wa mwaka wa kwanza kitivo cha sheria na elimu kugoma wakidai mikopo yoa kuwa tangu novemba mwka jana hivyo kusababisha kuishi kwa shida na kutopata mahitaji mihimu ya kila siku mgomo huo wa wanafunzi wa Makumira ulisababisha kufunga barabara kuu ya Arusha Moshi lazima watanzania tujiulize uko bodi kuna nini mbona kila kukicha mambo yanazidi kuwa mabaya.
Pia chuo kikuu kishiriki cha Tumaini Iringa wa wanafunzi wa kitivo cha elimu ya sanaa waligoma  kutoka na kutotambulika na TCU  kama kozi hii ipo katika chuo hiki na ivyo kusababisha wanafunzi hao kutopata mikopo yao  pamoja na migomo hii inayotokea katika vyuo mbalimbali laakini bado serikali inashindwa kutafuta mbinu mbadala ili kuepukana na  tatizo hili kwa linazidi kuwasugu kadri siku ziendavyo hapa nchi na katik migomo hiyo mingi imekuwa ikiongozwana vyuo vya serikali na vichache kutoka vyuo binafsi.
Hata ivyo migomo hii ikiendele kutulizwa katika vyuo vingine hali ikawa tata katika chuo cha Dar es salaam university college of  education baada ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kugoma kuingia darasani baada ya kucheleshewa mikopo yao katika hili serikali la itambue  ili iwezekujua mchawi na nani kati ya bodi ya mikopo na uongozi wa vyuo vikuu ambako migomo inatokea kila kukicha.
Pamoja na migomo hiyo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kila kukicha  lakini bado bodi inashindwa kuweka mambo sawa ili kufuta lawama wanazo pata kutoka kwa wanafunzi na watu mbalimbali kwasbabu migomo mingi inayotoke vyuo  lawama wana tupiwa bodi  ya mikopo.katika mgomo uliotokea katika chuo kikuu cha RUCO hivi karibuni  wnafunzi hao waligomo  kwasababu ya kucheleweshewa fedha za kujikimu na bodi ya mikopo.
Katika migomo hii yote inayotokea kwa sasa katika vyuo vikuu mbalimbali nchi lazima suala hili litafutiwe ufumbuzi ili kuweza kuepukana na tatizo hili kama tatizo ni bodi ya mikopo  nchini serikali ifanyie uchunguzi suala hili kwani bodi imekuwa ikitupiwa lawama kila kukicha kuwa wao ndio   cha cha migomo ya wanafunzi vyuoni.
Wanafunzi lazima watambue kuwa migomo sio suluhu ya matatizo ya kwani migomo hiyo husababisha baadhi ya kusosa masomo na wengine kufukuzwa vyuoni  na migomo hiyo inawezakuwasaidia wakatimiziwa mahitaji  yao kwa muda muafaka na villevile kutotimiziwa waliokuwa wanayahitaiji licha ya kwamba migomo hiyo ya wanafunzi husaidia kufichua yale mambo yaliyokuwa yamejificha vilevile kuhamasisha mabadiliko ambayo yanapelekea maendeleo katika vyuo vyao.

No comments:

Post a Comment